Kijiji chafunikwa na maporomoko,India


Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
 Jengo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.

Related Posts:

  • Ebola:Shule zote zafungwa Liberia Rais wa Liberia,Ellen Johson Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote nchini humo kama mpango wa taifa hilo wa kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ebola. Mpango huo pia unashirikisha kuzitenga baadhi ya jamii zil… Read More
  • Kijiji chafunikwa na maporomoko,India Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo. Kazi ya uokoaji inaend… Read More
  • Raisi Barack OBama kufikishwa mahakamani Atashtakiwa kwa kosa la matumizi mabovu ya madaraka chanzo: http://www.usatoday.com/story/news/politics/2014/07/29/president-obama-appeals-court-health-care-law/13316989/ … Read More
  • Tetemeko la ardhi China laua 380 Wafanyakazi wa Uokoaji nchini China wanaendelea kujitahidi kufikia eneo la lilipigwa na tetemeko la ardhi katika jimbo la Yunnan siku ya jumapili na kuua watu zaidi ya mia tatu na themanini. Kikosi cha dharura kinajaribu ku… Read More
  • Polisi akamatwa kwa wizi wa Cocaine Polisi wa Ufaransa wamemkamata afisa mmoja wa kukabiliana na mihadarati kwa kuiba kilo hamsini za Cocaine kutoka makao makuu ya polisi mjini Paris. Dawa hiyo yenye thamani ya dola millioni 4 ilikuwa imefungiwa katika chumba… Read More