Eto’o kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Chelsea na hivyo Liverpool wanataka kumpa mwaka mmoja wa kuichezea timu yao licha ya sasa kuwa kwenye hatua nzuri ya kumsainisha Mario Balotelli
SUPASTAA wa Cameroon, Samuel Eto’o amepewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na klabu ya Liverpool kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Eto’o kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Chelsea na hivyo Liverpool wanataka kumpa mwaka mmoja wa kuichezea timu yao licha ya sasa kuwa kwenye hatua nzuri ya kumsainisha Mario Balotelli.
Wakala wa Eto’o amekuwa akiwasiliana na klabu mbalimbali kwenye majira ya haya ya kiangazi kwa ajili ya mteja wake apate timu ya kucheza kufuatia kutemwa na Chelsea.
Imeripotiwa kwamba staa huyo wa Cameroon anataka kubaki kwenye Ligi Kuu England na hivyo kupata ofa hiyo ya mwaka mmoja Anfield ni jambo kubwa kwake.
Liverpool imepanga kumpa Eto’o mshahara wa Euro 93,000 kwa wiki na bonasi nyingine zitakazotokana na kiwango chake cha uwanjani.