Panga pangua, hii ndio Yanga mpya


IN SUMMARY
Kwa mujibu wa mazoezi yaliyofanyika Dar es Salaam na hapa Pemba jumlisha na mechi ya kirafiki waliyocheza, ‘First Eleven’ ya Yanga itakuwa kama ifuatavyo;
HII ni siri usimwambie mtu yeyote, uchune nayo hivyo hivyo kwa vile bado Marcio Maximo hajaweka wazi kikosi chake cha kwanza lakini tathmini ya Mwanaspoti imekibaini.
Kwa mujibu wa mazoezi yaliyofanyika Dar es Salaam na hapa Pemba jumlisha na mechi ya kirafiki waliyocheza, ‘First Eleven’ ya Yanga itakuwa kama ifuatavyo;
Kipa ni Deo Munishi ‘Dida’ kama kawaida na Juma Abdul atacheza beki ya kulia. Kushoto ni Oscar Joshua lakini Edward Manyama na Amos Abeil anaocheza nao nafasi moja ni hatari sana, Maximo anaweza akawatumia kwa kuchanganya kulingana na timu pinzani.
Beki ya kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kiungo mkabaji ni Mnyarwanda Mbuyu Twite na kiungo mshambuliaji ni Hassan Dilunga.
Panga pangua Mbrazili Andrey Coutinho atacheza winga ya kushoto na Mnyarwanda Haruna Niyonzima atacheza winga ya kushoto, mastraika wa kati ni Mrisho Ngassa anayecheza kama kiungo nyuma ya Genilson Santos Santana ‘Jaja’.
Kwenye nafasi za mbele, kiungo, winga na straika mambo yanaweza kubadilika kulingana na aina ya timu pinzani watakayocheza nayo.
Kwani wachezaji kama Simon Msuva anaweza kutumika kucheza winga ya kulia kama anataka timu icheze kwa kasi zaidi, Jerry Tegete, Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said Bahanuzi na Hussein Javu nao wanaweza kumpeleka Ngassa pembeni, kama atataka kucheza mpira wa kutulia.
Maximo amesisitiza kuwa katika mechi hizi za majaribio, anataka kuwatumia wachezaji wote ili awaone na ndivyo anavyowapa nafasi.
Ametengeneza ‘First Eleven’ mbili ambazo huchuana zenyewe kwa wenyewe na hao ndiyo watatoa kikosi halisi cha kwanza ambacho mwenyewe hajakiweka wazi.
“Kwa sasa nampa kila mchezaji nafasi ya kucheza, lengo ni kuwaona namna wanavyocheza na muunganiko wa kombinesheni ipi inakubali kupata kitu fulani kulingana na mechi,” alisema Maximo.
Maximo alitumia muda wa takribani robo saa akizungumza na wachezaji na baadaye walifanya mazoezi ya kukimbia na baadaye mafupi ya kucheza mpira.
Katika mazoezi hayo, kiungo Hassan Dilunga, alishindwa kufanya mazoezi na wenzake kwani alikuwa anasikia maumivu kwenye kidole cha mwisho cha mguu wa kulia kwani alijitonesha kwenye mechi ya juzi Alhamisi na Chipukizi.
Kiiza naye hakufanya kwa sababu alifiwa na kaka yake. Mwenyewe hakutaka kufafanua kwa undani kutokana na uchungu aliokuwa nao lakini inadaiwa kaka yake huyo aligongwa na gari.
Jaja aahidi makubwa
Straika Mbrazili, Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye amepachika bao la kwanza na pekee katika mechi yake ya kwanza timu yake ilipocheza na Chipukizi ya Pemba amechimba mkwara.
“Bao hili limenitia hamasa natamani ligi ianze hata sasa na ninachowaahidi mashabiki na wapenzi wa Yanga kila mechi kazi yangu itakuwa ni kutupia mabao tu,” alisema.
Akizungumzia kombinesheni ambayo yeye alicheza namba tisa na Mrisho Ngassa alicheza namba 10, Mnyarwanda Haruna Niyonzima alicheza winga ya kulia wakati Mbrazili Andrey Coutinho alicheza winga ya kushoto, Jaja alisema: “Ni kombinesheni nzuri kwangu, wananijulia na tutafanya makubwa zaidi.”

Related Posts:

  • matokeo ya mechi za premier league Aston Villa 0 - 0 Newcastle United Southampton 0 - 0 West Bromwich Albion Chelsea 2 - 0 Leicester City half-time: (0 - 0) match details : 63'Diego Costa 1, 77'Eden Hazard 2 Crystal Palace 1 - 3 West Ham United half-time: (… Read More
  • WENGER ASEMA MILANGO IPO WAZI KWA THOMAS VERMAELEN Kocha wa Arsenal , Arsene Wenger amethibitisha kwamba beki wake wa kati Thomas Vermaelen ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake huenda akaiama club hiyo maarufu kama wabeba mitutu wa london katika kipindi hiki cha… Read More
  • Panga pangua, hii ndio Yanga mpya IN SUMMARY Kwa mujibu wa mazoezi yaliyofanyika Dar es Salaam na hapa Pemba jumlisha na mechi ya kirafiki waliyocheza, ‘First Eleven’ ya Yanga itakuwa kama ifuatavyo; HII ni siri usimwambie mtu yeyote, uchune nayo hi… Read More
  • Eto’o kulamba mwaka mmoja Anfieldkwa ufupi Eto’o kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Chelsea na hivyo Liverpool wanataka kumpa mwaka mmoja wa kuichezea timu yao licha ya sasa kuwa kwenye hatua nzuri ya kumsainisha Mario Balot… Read More
  • Mechi za primier league leo tarehe 24/08/2014 ratiba ya mechi ziakazochezwa leo jumapili 24/8August 2403:30 Hull City Vs Stoke City03:30 Tottenham Hotspur Vs Queens Park Rangers06:00 Sunderland Vs Manchester United… Read More