Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.
Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa
Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa
wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua,
ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Utafiti
huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa
gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana
katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya
magonjwa.
"Ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na
harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya
mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa
fulani,'' anasema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Watafiti
wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo
mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile,
Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa