CCM KURIDHIA KUENDELEA KWA BUNGE LA KATIBA


Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, chama tawala nchini Tanzania, jana jioni imehitimisha mkutano wake maalumu wa siku moja na kuridhia kuendelea kwa bunge la katiba ambalo limekuwa likilalamikiwa kufanyika kinyume na taratibu na baadhi ya kundi lijiitalo UKAWA lililojiengua katika vikao vya bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma. Mkutano huo ulikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM, rais Jakaya Mrisho Kikwete.