Kikosi cha wapiganaji wa kiislam wenye msimamo mkali
Islamic State kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari
mwenye asili ya Marekani aliyetekwa nyara nchini Syria 2012.
James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.Katika video hiyo mwandishi huyo wa kujitegemea anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''
anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.
Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa ’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya mabomu yanayowalenga wa Iraq.