Muingereza mwenye Ebola arejeshwa kwao

Maafisa wa serikali ya Uingereza wanasema kuwa mfanyakazi mmoja wa utabibu kutoka Uingereza ambaye ameambukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, ataletwa Uingereza.
Mkaguzi wa ebola katika hospitali ya Sierra Leone
Atasafirishwa kwa ndege ya jeshi la wanahewa la Uingereza.
Atatibiwa kwenye kituo kilichotengwa ndani ya hospitali moja mjini London.
Afisa wa wizara ya afya ya Sierra Leone alisema mwanamme huyo amekuwa akifanya kazi katika kituo cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi.