Polisi akamatwa kwa wizi wa Cocaine

Polisi wa Ufaransa wamemkamata afisa mmoja wa kukabiliana na mihadarati kwa kuiba kilo hamsini za Cocaine kutoka makao makuu ya polisi mjini Paris.
Dawa hiyo yenye thamani ya dola millioni 4 ilikuwa imefungiwa katika chumba kimoja baada ya polisi kuipata na genge moja la raia wa Senegal linalofanya oparesheni zake katika mji huo.

katika kesi ambayo imeiletea aibu serikali ya Ufaransa ,polisi walibaini siku ya Alhamisi kwamba dawa hizo zilikuwa zimetoweka katika makao makuu ya polisi.Maafisa wanasema kuwa afisa huyo mwenye umri wa miaka 34 alisakwa na kukamatwa katika mji wa kusini wa Perpignan ambapo alikuwa likizo.
Taarifa ya polisi inasema kuwa kanda ya video ya CCTV iliomuonyesha mtu mmoja aliyebeba mifuko miwili akiingia katika makao hayo na baadaye akaonekana akitoka na mifuko hiyo.
Afisa huyo mwenye umri wa miaka 34 alipatikana katika mji wa Perpignan ambapo alikuwa akijivinjari.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ufaransa Bernard Cazenueve ambaye amesema kuwa atakabiliana na waliokamatwa bila huruma iwapo itabainika kwamba baadhi ya maafisa walihusika aamesema kuwa afisa huyo tayari amesimamishwa kazi akisubiri uchunguzi.
Mnamo mwezi Aprili maafisa wawili wa polisi walishtakiwa kwa kumbaka mwanamke mmoja raia wa Canada katika jengo hilo.

Related Posts:

  • Kobe aliyepotea akamatwa na polisi huo Los Angeles ALHAMBRA, Calif. (AP) -- At least officers didn't have to cite it for speeding when the Alhambra Police Department pulled over a giant tortoise found wandering on a local street. Police say the hard-shelled reptile was nab… Read More
  • Kijiji chafunikwa na maporomoko,India Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo. Kazi ya uokoaji inaend… Read More
  • Polisi akamatwa kwa wizi wa Cocaine Polisi wa Ufaransa wamemkamata afisa mmoja wa kukabiliana na mihadarati kwa kuiba kilo hamsini za Cocaine kutoka makao makuu ya polisi mjini Paris. Dawa hiyo yenye thamani ya dola millioni 4 ilikuwa imefungiwa katika chumba… Read More
  • Ebola:Shule zote zafungwa Liberia Rais wa Liberia,Ellen Johson Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote nchini humo kama mpango wa taifa hilo wa kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ebola. Mpango huo pia unashirikisha kuzitenga baadhi ya jamii zil… Read More
  • Ajali ya ferri ferry iliyokuwa imebeba abiria takribani 200 imezama katika mto kusini mwa mjimkuu Dhaka. Ripoti zinasema takribani abiria 50 wameokolewa… Read More