Tetemeko la ardhi China laua 380

Wafanyakazi wa Uokoaji nchini China wanaendelea kujitahidi kufikia eneo la lilipigwa na tetemeko la ardhi katika jimbo la Yunnan siku ya jumapili na kuua watu zaidi ya mia tatu na themanini.
Kikosi cha dharura kinajaribu kukarabati barabara zilizoharibiwa ili kuwezesha usafiri katika maeneo yaliyopata mvua kubwa na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.
Maelfu ya watu waliodhurika na tetemeko hilo wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa na mamlaka zinazohusika.
Shuhuda mmoja amesema karibu theluthi mbili ya nyumba zimeharibiwa katika kijiji chao.
Maelfu ya mahema na vitanda vya dharura vimepelekwa katika eneo hilo liloathirika na maelfu ya wafanyakazi wa idara ya dharura watumwa kusaidia kazi ya uokoaji.
tetemeko la ardhi nchini China

Related Posts:

  • Muingereza mwenye Ebola arejeshwa kwao Maafisa wa serikali ya Uingereza wanasema kuwa mfanyakazi mmoja wa utabibu kutoka Uingereza ambaye ameambukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, ataletwa Uingereza. Atasafirishwa kwa ndege ya jeshi la wanahewa la Uin… Read More
  • IKULU YA MAREKANI YAVAMIWA A man jumped over the White House fence on Wednesday night, but this time, the man barely made it onto the lawn before being taken down by a K-9 and quickly detained by Secret Service agents.… Read More
  • DRC: Watu wawili wafa kwa Ebola Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo. Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa nje ya Afrika Magharibi tang… Read More
  • Mateka waendeshwa kwata Ukraine Wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine wanaoipendelea Urusi wamewaendesha kwata katika barabara za mji wa Donetsk, wanajeshi kadha wa Ukraine waliowateka. Donetsk ni ngome ya wapiganaji hao. Mambo hayo yamejiri siku ya kuadhi… Read More
  • Boko Haram yatangaza himaya yao Nigeria Kundi la wanamgambo wa Boko Haram limesema kuwa limebuni taifa la kiislamu katika miji na vitongoji inavyotawala kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video il… Read More