

Marco Reus, 25, wa Borussia Dortmund, ambaye anafuatiliwa na Manchester United na Liverpool (Sunday Express), meneja wa Swansea Gary Monk amesema mshambuliaji wake Wilfried bony, 25, haondoki, licha ya Liverpool kumuulizia (Talksport), hata hivyo Tottenham wanamtaka pia Bony na vilevile kiungo Morgan Schneiderlin wa Southampton, na wawili hao huenda wakagharimu pauni milioni 45 (Sunday Mirror), Real Madrid huenda wakamchukua kipa wa Chelsea Petr Cech, iwapo Thibault Cortois, 22, atakuwa namba moja Darajani (Sunday Telegraph), mshambuliaji wa Manchester City john Guidetti, 22 aliyekuwa kwa mkopo Feyenoord, huenda akajiunga na Ajax, kwa kuwa hahitajiki Etihad (Mail on Sunday), meneja wa Aston Villa Paul Lambert atakuwa na mazungumzo na beki Ron Vlaar, 29 baada ya Juventus kutaka kumsajili (Sun), beki wa Atlètico Madrid, Javier Manquillo, 20 anajiandaa kufanya vipimo vya afya Liverpool kukamilisha uhamisho wa mkopo wa miaka miwili (Liverpool Echo), mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie, 30, atakosa kucheza mwanzo wa msimu akiendelea kupumzishwa baada ya Kombe la Dunia (Sunday People), meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema "alishangazwa" na magoli manne ya Yaya Sanogo wakati Gunners waliposhinda 5-1 dhidi ya Benfica katika Kombe la Emirates (Mail on Sunday), meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema Frank Lampard, 36, ambaye atajiunga na Manchester City kwa mkopo, kutoka New York City FC, na Ashley Cole, 33, aliyejiunga na Roma, wote walipewa mikataba mipya Darajani (Daily Star), Thomas Vermaelen atasaini mkataba na Barcelona kutoka Arsenal. Louis van Gaal alikuwa akimtaka beki huyo, lakini atasaini mkataba wa pauni milioni 10 (Daily Mirror), Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho (Daily Star). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. cheers!